SHAMSA AMFUNDA SHILOLE SIRI YA NDOA
Staa wa Filamu nchini, Shamsa Ford amefungukia uamuzi wa msanii mwenzake wa Muziki, Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole kwa kuamua kufunga ndoa tena ya Kidini na mpenzi wake, Uchebe ndoa iliyoshuhudiwa hivi karibuni na kutikisa kwenye mitandao na vyombo vya habari huku ikiwaacha midomo wazi kwa wale walidhani kuwa angerudiana na mpenzi wake wa zamani, Nuh Mziwanda.
Shamsa ambaye pia alifunga ndoa mwaka huu na mpenzi wake, Chidi Mapenzi ametumia ukurasa wake wa Instagram kumsihi Shilole atulie, aweke umaarufu pembeni, aitunze ndoa yake na hatimaye atafaidi matunda ya ndoa iliyo bora.
Shamsa ameandika;
“Hongera sana mamy. Umefanya maamuzi sahihi ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.Cha muhimu uwe mke bora wa Kitanzania kwa mumeo na ustar uweke pembeni.
“Mumuweke Mungu mbele, uvumilivu na kuheshimiana inshaallah mtazikana.Karibu kwenye Chama mama….Sasa nyie mnao subili matajiri wawaoe wakati hao matajiri wana wake zao wameanza nao moja mtasubili sana mpaka uso uote sugu.Uzuri na Ustar una mwisho wake. Iitafika muda hata inzi hakusogelei……HONGERA MAMA @shilolekiuno_badgirlshishi,” ameadika Shamsa.
No comments