BARAKA DA PRINCE NDIO BASI TENA
Habari wakuu,
Kufa kimuziki kwa Baraka da prince wap alikosea?
Kama nlivyotangulia hapo awali swala la anguko la baraka kimuzik alilisababisha mwenyewe kwa haya machache ambayo aliyafanya;-
1. Ku-side team kati ya upande wa kiba na diamond, hii ilikua ishara mbaya sana kwake kwa siku za usoni, kwan msanii wa level zake hakupaswa kuwagawa mashabiki zake..
Badala yake hakupaswa kujionyesha wazwaz yuko upande gan ijapokua kikawaida ilikua inajulikana yuko upande wa kiba kwa kua walikua 'lebel mates'
Lakini kitendo cha kujinasibu hadharan kupitia mitandao ya kijamii ndo alikua anapanda mbegu ya anguko lake pasi na kujua.
2. Kupishana na upande wa team ambayo alikua anachezea..
yan kuznguana na kiba pamoja na rockstar kwa ujumla, mbegu nyingne akaotesha kwenye mgongo wa dunia..
Kwan pale awali wakat yuko upande wa kiba team diamond karibia wote hawakua wakimpenda so, ni kama alikua na mashabik wa upande wa kiba plus wale ambao hawana team..
Hivyo kitendo cha kukorofishana na kina kiba kukamfanya apoteze kotekote'
Yaani neither team Diamond nor team Kiba..na ukiacha hao jamaa wawili mashabiki wanaobak kimuziki hawana nguvu sana kwan muzik wa sasa ni wa promotions sana na mashabiki wa hzo team mbili wako vzur kwenye hilo (hapo nazungumzia mitandao ya kijamii) na bila trending ya kwenye social media muzik wa leo hutoboi.
3. Hili swala la tatu ndo lililompa sana baraka kiburi..
Alikua anaamini sana kuwa ukiwa na kipaji hakuna atakaekusumbua..so kipaji chake ndo kilichomfanya avimbe (bila shaka ni kweli he's talented) tena sana..
Akasahau kua:-
Bongo hatu-HIT kwa vipaji
Bali nani anabeba FLASH ya singo yako kupeleka kwenye Media houses.
Lakini pia hakujua kama mashabiki wanalamishwa kuamin flan anafanya muzik mzur hata kama siyo kweli na mifano tunayo tena hai kabisa..
Na laiti kama wananchi ndo wangekua waamuzi wa kuwaweka kileleni wasanii wenye talanta basi mtu kama Belle9, Rubby, mayunga na wengine kibao wasingepotea..
Yawezekana hayo yote hakuyajua' mfano saiz katoa nyimbo zaidi ya moja lakini zmepotelea studio2 "sometimes" ni bonge la wimbo ambao hauna hata miezI miwili lakini umepotea kwenye mzunguko..
Karibu umshauri huyu kijana kipaji kisipotee huku kinaonekana..
No comments