Polepole Aliamsha Dude Amtaja Kikwete, Lowasa Kuhusu Babu Seya na Mwanaye "Lowasa Halishindwa Kumshawishi Kikwete Ili Awatoe"
Humphrey Polepole ameibuka na kusema kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya nne Edward Lowassa alishindwa kuzuia Babu Seya asifungwe na kudai pia alishindwa mshawishi Mhe. Jakaya Kikwete ili awatoe watu hao.
Polepole amesema hayo baada ya watu kuanza kusema kuwa jambo alilofanya Rais Magufuli kuwatoa Babu Seya na mwanaye Papi Kocha ni jambo ambalo Lowassa aliahidi katika kampeni zake za 2015 kuwa endapo angechaguliwa kuwa Rais wa Tanzania angewaachia huru watu hao.
"Huyu mzee ambaye amezungumza kwamba hii ilikuwa ahadi yake kipindi cha kampeni ni mzee ambaye amehudumu kwenye serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kipindi ambacho Babu Seya anafungwa huyu mzee alikuwa Waziri Mkuu mwenye nguvu sana, kama alijua Babu Seya labda hakutendewa haki kwa namna yoyote kwa fikra zake angaliweza kumshauri Rais wake kipindi hicho kwamba huyu mtu hastahili kufungwa asamehewe" alisema Polepole
Polepole aliendelea kusisitiza kuwa Lowassa alishindwa kuzuia Babu Seya na watoto wake wasifungwe "Kashindwa kuzuia Babu Seya asifungwe, kashindwa mwaka wa kwanza kumshawishi Rais wake amsamehe Babu Seya, ameshindwa kufanya hivyo kwa miaka mingi iliyopita. Magufuli hakuwa kwenye nafasi ya uamuzi kipindi hicho alikuwa Waziri wa kawaida kabisa baada ya tafakuri ya kina ya miaka miwili akaona katika watu ambao wamejirudi huyu anastahili msamaha, huyo mzee anaibuka oohh nilifanya mimi, huyu mzee aache hizi tabia za kinafiki, kizandiki kwani Watanzania wanataka upinzani unaojenga hoja" alimalizia Polepole.
Babu Seya na mtoto wake Papii Kocha waliachiwa huru katika kifungo cha maisha jela baada ya Rais John Pombe Magufuli kuwapa msamaha katika siku ya Uhuru wa Tanzania bara, ambapo kila mwaka Disemba 9 zinafanyika sherehe za kumbukumbu.
No comments