Breaking News

MUGABE AONDOKA ZIMBABWE TANGU AONDOLEWE MADARAKANI  


Aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameondoka nchini humo kwa mara ya kwanza tangu alipoondolewa madarakani na jeshi ambapo  amesafiri kwenda Singapore kwa matibabu.

Kwa mujibu wa maafisa wa usalama wa serikali ambao wamezungumza na Reuters, Mugabe, 93, aliondoka nchini humu kwa ndege kutoka mjini Harare.

Aidha Mzee Mugabe Aliambatana  na mke wake Grace na wasaidizi kadha na Anatarajiwa kutua mjini Malaysia ambapo binti yake  Bona yupo akiwa ni  mjamzito.

Mugabe, aliyekuwa ameongoza taifa hilo kwa miaka 37, alijiuzulu baada ya jeshi likishirikiana na baadhi ya maafisa wakuu wa chama tawala cha Zanu-PF kumgeuka ilipobainika kwamba alikuwa anamuandaa Grace, 52, awe mrithi wake.

Safari hiyo ina maana kwamba Mugabe huenda hatakuwepo nchini Zimbabwe chama cha Zanu-PF kitakapokuwa kinamuidhinisha rasmi Rais Emmerson Mnangagwa kuwa kiongozi wa chama na mgombea urais wa chama hicho uchaguzi wa mwaka ujao.

Chama hicho kinatarajiwa kuandaa mkutano wake mkuu Ijumaa.

Maafisa wa usalama hawajasema Mugabe alisafiri vipi lakini gazeti la kibinafsi la NewsDay limeripoti kwamba alisafiri kwa ndege ya shirika la serikali la Air Zimbabwe.

No comments