Breaking News

MSIGWA AWAVAA VIONGOZI WA CCM

Mbunge wa Iringa Mjini  CHADEMA, Peter Msigwa amewavaa baadhi ya viongozi wa CCM ambao wamekuwa wakisema upinzani Tanzania unakufa na kuwahoji kuwa endapo upinzani ukifa ndiyo maendeleo ya nchi yatapatikana.

Msigwa amesema hayo jana kupitia ukurasa wake wa Facebook baada ya juzi baadhi ya viongozi wa CCM waliokuwepo kwenye Mkutano Mkuu UVCCM wa 9 ambao ulifanyika mjini Dodoma Disemba 10, 2017 ambapo wapo baadhi ya wanachama na viongozi wa chama hicho walikuwa wakisema kuwa kwa sasa upinzani nchini unakufa.
"Mkutano wa UVCCM ulibebwa na kibwagizo cha upinzani kuwa unakufa ! Fine, tukubaliane kuwa upinzani unakufa! Ukifa upinzani zitaongezeka ajira ngapi! Umaskini utapungua kwa kiwango gani? Haki za binadamu zitalindwa kwa kiwango gani? Utawala bora utaimarika kwa kiwango gani ? Demokrasia itaimarishwa kwa kiwango gani? Uhuru wa kutoa mawazo na vyombo vya habari utaimarika kwa kiwango gani! Haya yote hayana chama! Nilitegemea CCM mje namajibu ya haya sio upinzani unakufa"alisisitiza Msigwa.

No comments