MRISHO GAMBO ASEMA LEMA YUPO MBIONI KUHAMIA CCM
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo jana Disemba 10,2017 ameweka picha kwenye mtandao wake wa Facebook akiwa na Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Godbless Lema na kusema kuwa yupo mbioni kurudi nyumbani.
Baada ya kuweka picha na ujumbe huo baadhi ya watu walianza kusema kuwa Mkuu wa mkoa huyo anafanya siasa rahisi huku wengine wakisema ni jambo ambalo haliwezekani Mbunge huyo wa CHADEMA kurudi CCM ili hali wapo ambao wanatamani jambo hilo litokee hata leo.
"Msituko. Yupo mbioni kurudi nyumbani" aliandika Mrisho Gambo
Haya ni baadhi ya maoni ya watu katika mtandao wa Facebook wa Mrisho Gambo baada ya kuweka picha akiwa na Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA.
No comments