Breaking News

Wabunge watatu CHADEMA watimba TAKUKURU

Wabunge wa CHADEMA akiwepo Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa wamefika Ofisi za Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa jijini Dar es Salaam kutoa ushahidi.

Wabunge hao jana baada ya kutoa ushahidi kuhusu wateule wa Rais kuwanunua baadhi ya madiwani wa CHADEMA waliahidi kwenda kwenye taasisi hiyo ya kupambana na rushwa ili kuwapa ushahidi mwingine ambao walishindwa kuutoa mbele ya waandishi wa habari kwa kuhofia kuleta taharuki zaidi juu ya ushahidi huo. 

No comments