Breaking News

Video: Dereva wa Rais wa Marekani akifanya mazoezi ya kuendesha gari

Rais wa Marekani ni miongoni mwa viongozi duniani ambapo ulinzi wao ni imara sana ambapo anaposafiri ndani ama nje ya nchi, huambatana na watu wa aina mbalimbali ambao lengo lao kuu ni kuhakikisha kwamba anakuwa salama wakati wote.
Rais yeyote wa Marekani, anaposafiri hutumia gari maalumu la Rais ambapo wakati akiwa ndani ya gari hilo hutambulika kama Cadillac One au maarufu zaidi kwa jina la The Beast.
Gari hili ni maalum sana kutokana na namna lilivyotengenezwa ili kuhakikisha usalama wa Rais wakati wote bila kujali linapitia mazingira gani.
Miongoni mwa vitu vya kipekee zaidi ambavyo vimo kwenye gari hilo ni pamoja na damu ambayo inafafana na kundi la damu la Rais endapo kutatokea tatizo na atahitaji kuongezewa damu, kuna hewa ya oksijeni kwa ajili ya Rais kupumua, gari hilo lina mifumo ambayo husaidia kuzuia makombora yaliyorushwa kulilenga.
Mbali na hayo, gari hilo haliruhusu risasi kupita, tairi zake ni imara sana kwa namna ambayo si rahisi kupasuka kirahisi, na hata zikipasuka, gari hilo litaweza kuendelea kwenda. Pia mawasiliano ya gari hili yameunganishwa na satelaiti ili kuhakikisha muda wote Rais anakuwa na mawasiliano na Pentagon, na pia, dumu la mafuta la gari hilo, limetengenezwa kwa namna kwamba haliwezi kulipuka.
Kuhusu dereva wa gari hilo, ni miongoni mwa usalama wa taifa na huwa na mafunzo maalumu kwa ajili kumuendesha Rais.
Dereva huyo hufanya majaribio magumu sana, yakiwemo kuendesha gari katika barabara mbovu, kuendesha gari kwa kasi ya juu, kuendesha gari kasi kwa kurudi nyuma pamoja na mambo mengine ambayo yatamfanya aweze kumuokoa Rais akiwa salama endapo tatizo la kiusalama litatokea.
Hapa chini ni video za madereva wa Rais wa Marekani wakifanya mazoezi ya kumuendesha Rais.


No comments