Mkuu wa Mkoa Abadilishiwa Kituo cha Kazi Akiwa Ikulu na Rais Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amebadilishia kituo cha kazi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma aliyeapishwa leo, Bi. Christine Mndeme na kumpangia kuwa mkuu wa mkoa Ruvuma.
Bi Christine alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma na jana aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma . Kwahiyo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge kwasasa atahamia Mkoa wa Dodoma na nafasi yake itachukuliwa na Christine Mndeme.
Rais Magufuli leo mchana amewaapisha Makatibu Wakuu wapya, Naibu Makatibu Wakuu wapya na Wakuu wa Mikoa wapya baada ya jana kuwateua.
Hata hivyo Rais Magufuli amemtaka kiongozi huyo kwenda Mkoani humo kuhangaikia changamoto ya barabara mkoani humo.
No comments