Breaking News

Majeruhi wa shambulizi la Mogadishu wasafirishwa Uturuki kwa matibabu

Takriban watu 30 wamesafirishwa kwenda nchini Uturuki kupata matibabu ya dharura, kufuatia shambulizi la bomu la siku ya Jumamosi lililotegwa ndani ya lori kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu. 

Zaidi ya watu 300 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa kufuatia shambulizi hilo, Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika kwenye shambulizi hilo. 

Hilo ndilo shambulizi baya zaidi kutokea nchini Somalia tangu kundi la al-Shabab lianzishe harakati zake mwaka 2007. 

Rais Mohamed Abdullahi "Farmajo" Mohamed alilaumu kundi la al-Shabab kwa shambulizi hilo katili. 

Reuters walimnukuu Ahmed Ali, muuguzi anayefanya kazi kwenye hospitali moja akisema kuwa miili 160 haikuweza kutambuliwa na hivyo ilizikwa na serikali jana, Anasema kuwa miili mingine ilizikwa na jamaa zao. 

No comments