Breaking News

Klabu ya Yanga Yazindua Magazine Yake Leo


Klabu ya soka ya Yanga hii leo imezindua rasmi Magazine yake ikiwa imesalia siku moja kabla ya mchezo wao wa Dar es salaam Darby dhidi ya hasimu wake Simba SC ikiwa na lengo la kujiongezea kipato.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram wa klabu ya Yanga hapo jana imeeleza kuiingiza rasmi sokoni Magazine hiyo hii leo siku ya Ijumaa.

Tunapenda kuwataarifu wanachama, mashabiki na wadau mbalimbali wa soka kuwa ‘Yanga Magazine’, itaanza kuuzwa rasmi kesho (Ijumaa) kuanzia saa 3:00 Asubuhi Makao Makuu ya Klabu.

Hata hivyo jarida hilo litaanza kuingia mitaani leo jioni badala ya asubuhi kama ilivyokusudiwa kutokana na matatizo ya umeme.

No comments