Breaking News

Kilichoendelea Leo Mahakamani Katika Kesi ya Agnes Masogange

Upande wa utetezi wa kesi ya kutumia dawa za kulevya inayombili msanii, Agnes Gerald maarufu kama Masogange utaanza kutoa ushahidi Novemba 14, 2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mshtakiwa huyo alipaswa kuanza kujitetea leo Alhamisi lakini Wakili wa Serikali, Adolf Mkini aliomba kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ipangiwe tarehe nyingine.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Mashauri aliiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 14, 2017.

Hatua hiyo imefikiwa mara baada ya Hakimu Mashauri kumuona mshtakiwa huyo kuwa ana kesi ya kujibu na kwamba anapaswa kujitetea na kuwaita mashahidi wake.

Masogane anatetewa na mawakili Nehemia Nkoko na Ruben Simwanza.

Kesi hiyo inaendeshwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula ambaye kwa upande wao kuwaita mashahidi watatu wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao na kuufunga.

Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.

Anadaiwa kufanya makosa hayo chini ya kifungu cha 18 (a) cha Sheria ya Kupambana na Dawa za Kulevya namba 5 ya mwaka 2015.

No comments