Breaking News

HUYU HAPA POGBA MAN UNITED


England.HABARI njema kwa mashabiki wa Manchester United baada ya kiungo wao ghali, Paul Pogba kurudi na kuonekana mazoezini huko Carrington.

Pogba alionekana kwenye uwanja wa mazoezi wa Man United, ambayo inajiandaa kwa ajili ya kuwakabili Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa Ligi Kuu England utakaofanyika kesho Jumamosi huko Old Trafford.

Staa huyo Mfaransa amekuwa nje ya uwanja tangu mapema mwa mwezi uliopita baada ya kupata majeruhi kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Basel.

Pogba alitarajiwa kurejea uwanjani kwenye mechi dhidi ya Swansea City kwenye Kombe la Ligi Jumanne iliyopita, lakini Man United ilifikiria kumpa matibabu zaidi ili apone kwa uhakika na si kumharakisha kurudi uwanjani.

Siku za karibuni, kiungo huyo alikuwa huko Miami, Florida kufanya mazoezi ya kujiweka fiti, lakini staa wa Man United, Jesse Lingard, ambaye ni swahiba mkubwa wa Pogba jana Alhamisi alituma video kwenye ukurasa wake wa Instagram akimwonyesha Pogba kwamba amerudi Manchester kabla ya kiungo huyo kuonekana akitembea bila ya matatizo yoyote kwenye korido za uwanja wa mazoezi wa Carrington, ambako Man United inajifua kwa nguvu zote kwa ajili ya kuikabili Spurs ya Mauricio Pochettino kwenye dimba la Theatre of Dreams. Wakati huo huo, Eric Bailly naye amerudi mazoezini baada ya kuwa nje ya uwanja kwa mwezi mzima.

Wachezaji Ander Herrera na Marcus Rashford nao walipata majeraha madogo kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Swansea City Jumanne iliyopita, lakini nao walikuwapo mazoezini.


No comments