NGOMA MPYA YA ALLY KIBA IKO TAYARI
Msanii wa Bongo Flava, Alikiba huenda akatoa ngoma mpya muda wowote.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma Seduce Me katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ameandika ujumbe ambao kwa kiasi fulani unahashiria ujio wa ngoma mpya.
Ujumbe huo ambao ulilenga kumpongeza msanii mwenzake, Abby Skillz kwa kufunga ndoa uliishia kwa kudokeza hilo.
Hongera Mkongwe nakutakia Kheri Na mafanikio Katika Ndoa Yako
Na ngoma Mpya Inafuata
#SapportedByKiba
#KingKiba
Hata hivyo haijaeleweka iwapo ngoma hiyo itakuwa ya Abby Skillz pekee kwani amekuwa akifanya kazi na Alikiba kupitia King’s Music. Ikumbukwe wawili hawa walishatoa wimbo pamoja mwaka jana ‘Averina’ ambao Mr. Blue alishirikishwa pia.
Wiki mbili zilizopita katika mahojiano na Bongo5 Alikiba alisema ngoma yake ‘Seduce Me’ ikifikisha views milioni 10 katika mtandao wa YouTube atatoa ngoma mpya. Hadi kufikia sasa ngoma hiyo ina views milioni 6.1
No comments