Breaking News

Hans Poppe afunguka haya baada ya kiongozi wa Yanga kuchaguliwa kuiongoza Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara

Mwenyekiti wa usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hans Poppe amesema mwenyekiti mpya wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania bara (TPLB) Clement Sanga atende haki katika uongozi wake bila kujali kuwa yeye ni kiongozi wa Yanga.

“Yeye kuipenda Yanga hatumzuii kwa sababu ni mpenzi wa Yanga na kiongozi kule lakini atende haki asijipendelee”-Hans.

“Sasa hivi tunataka maendeleo ya soka sio mambo ya longolongo. Clement Sanga ni mtu ambae namfahamu nimezungumza nae mara kwa mara kwa mtazamo wake ni mtu ambae anapenda maendeleo nina imani atatekeleza wajibu wake vizuri.”

“Nimshauri tu kama kuna mambo anatakiwa ayasikilize wao kama rufaa basi wafanye ndani ya muda na kusimamia ratiba isibadilishwe mara kwa mara.”

Sanga ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa klabu Yanga amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania bara akimwangusha Ahmed Yahaya aliyekuwa madarakani awali kabla ya uchaguzi kufanyika.

No comments