Breaking News

CCTV Camera imeondolewa kwenye eneo alikopigwa risasi Tundu Lissu – Mbowe

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe amesimama leo na kuongea tena kuhusu ishu ya Tundu Lissu kuanzia tukio lenyewe mpaka afya yake ya sasa kama alivyonukuliwa na kauli zake kuandikwa hapa chini.

1. Tunaamini kabisa waliomdhuru Lissu wapo na wanajulikana na Serikali, vyombo vya ulinzi na usalama vinajua nani amemshambulia Lissu, jambo hili limetendwa na vyombo vya Serikali na kwenye hili hatumumunyi maneno.

2. Shambulio dhidi ya Lissu limetendwa mchana kweupe katika makazi ambayo Viongozi wa serikali wanakaa, makazi ambayo kuna camera za kuchukua matukio yote yanayotokea, makazi ambayo kuna Askari wanalinda saa 24 na silaha, haiwezekani mtu akashambuliwa saa 7 mchana.

3. Tundu Lissu anakaa jirani na Waziri, kwenye nyumba ya Waziri kuna camera ya CCTV ambapo taarifa zetu za kiuchunguzi zinaonyesha ile camera imeondolewa, imeondolewa na nani? kwasababu gani na imepelekwa wapi?

5. Limeanzia kwa Lissu na kuna wengine miongoni mwetu tuko kwenye WANTED LIST, huu ni utamaduni ambao hatukuuzoea kwenye nchi yetu kwahiyo hatuwezi kulichukulia kama jambo jepesi la kuitwa, kaeni chini tuwape fedha…. hapana, japo tunahitaji fedha…. tunahitaji kwanza haki yetu ya kuishi.

6. Misimamo ya chama chetu haitoyumbishwa na fedha zozote zile……. pamoja na umasikini wetu, tunajali zaidi ulinzi wetu na wa kila Mtanzania apate haki yake.

7. Kuna lawama kwamba Dereva wake anahusika… sawa yeyote ahusike hatuna tatizo lakini ambacho tumesisitiza na tunashangaa kwanini Serikali inapata kigugumizi Wachunguzi wa Kimataifa kuja Tanzania.

8. Hatuna imani na vyombo vyetu vya dola vya ndani sio kwasababu havina uwezo bali ni kwasababu havina dhamira, naomba ieleweke hatudharau kabisa vyombo vyetu vya ndani ila tunajua vinafanya kazi kwa mashinikizo ya viongozi vya Serikali… vyombo vyetu vya dola ni tawi la Chama cha Mapinduzi.

No comments