Breaking News

Alichosema Kikwete yanayoendelea nchini

Mbunge wa jimbo la Chalinze (CCM) Ridhiwani Kikwete amefunguka na kutoa ushauri wake kwa mambo ambayo yanaendelea hivi sasa nchini kwa kusema muda mwingine kabla ya kukosoa ni bora tuwe tunapongeza ili kuwapa nguvu viongozi.

Ridhiwan Kikwete amesema hayo kupitia mtandao wake wa Instagram baada ya kuweka picha ya Rais John Pombe Magufuli na kuambatanisha nukuu ya Rais wa tatu wa Marekani Thomas Jefferson ambaye alitawala mwaka  1801 mpaka 1809 ambayo ilikuwa inasema. 

“Mengi nimeyasoma yaliyoandikwa, mengi nimeyasikia toka kwa wachambuzi. Wakati mwengine ni Vyema tukajenga Taifa la watu ambao kabla hamjakosoa, tunapongeza kwa mafanikio tuliyoyapata ili kuwapa nguvu wale tuliowapa dhamana ya kutupigania.”  

Ridhiwan Kikwete ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Serikali kutoa taarifa kuwa wamekubaliana na Barrick Gold Mining juu ya mambo kadhaa ikiwa pamoja na kampuni hiyo kukubali kuilipa Tanzania dollar milioni 300 badala ya dollar milioni 880 ambayo ingelipwa kama 'capital gains tax" jambo ambalo limeibuka mijadala mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii. 

No comments