Breaking News

WAZIRI UMMY ATOA MAAGIZO HAYA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu

Sekretarieti hizo kuhakikisha na kuhimiza ujenzi wa nyumba bora.Halmashauri zihimize usafi wa mazingira kwenye maeneo yao.Kudhibiti uingizaji na matumizi ya mitambo na magari chakavu.

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameziagiza sekretarieti za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kusimamia utekelezaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi ikiwemo kupanga maeneo ya makazi, viwanda na ujenzi wa madampo ya kisasa kwa ajili ya kutupa taka.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Jumanne kuhusu maadhimisho ya Siku ya Afya ya Mazingira, Ummy amezitaka sekretarieti hizo kuhakikisha na kuhimiza ujenzi wa nyumba bora huku akizitaka zijengwe katika maeneo rasmi.

Amesema pamoja na mambo mengine, ngazi zote za halmashauri zihimize usafi wa mazingira kwenye maeneo yao na kudhibiti uingizaji na matumizi ya mitambo na magari chakavu.

“Ninaziagiza sekretarieti za mikoa na mamlaka ya serikali za mitaa kuhakikisha mnasimamia sheria za udhibiti wa uchafuzi wa hewa na kila kiwanda kinakuwa na mitambo ya kudhibiti uchafuzi wa hewa lakini pia mnapaswa kuhamasisha ubunifu na matumizi ya teknolojia ya nishati mbadala,”amesema.

No comments