TSHABALALA YAMKUTA MAZITO SIMBA
Beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.
AMA kweli hakuna ufalme unaodumu milele!Beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ alikuwa kama mfalme wa nafasi ya kushoto msimu uliopita pale Simba na aliweka rekodi ya kucheza mechi zote za ligi, lakini mambo yamebadilika msimu huu, amepata mpinzani na amepigwa benchi mechi mbili mfululizo kwenye ligi.
Juzi Simba ilicheza dhidi ya Azam FC kwenyeUwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Darna kutoka suluhu. Tshabalala alikuwa benchi.
Tshabalala hadi sasa ameshindwa kufua dafu mbele ya beki mpya wa timu hiyo, Erasto Nyoniambaye amejiunga na klabu hiyo hivi karibuni akitokea Azam FC.
Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog amekuwa akimpatia Nyoni nafasi ya kucheza kila wakati kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa tangu alipojiunga na timu hiyo.
Akimzungumzia mchezaji huyo, Omog alisema: “Nyoni ni mchezaji mwenye faida kubwa anapokuwa uwanjani, mbali ya kucheza nafasi ya beki wa kushoto lakini pia ana msaada mkubwa kwa mabeki wa kati na pindi tunapokuwa tunashambuliwa.
“Anajua kukaba vizuri lakini pia anajua kuanzisha mashambulizi, kwa hiyo ni mtu muhimu sana katika kikosi changu.
“Kuhusu Tshabalala ni mchezaji mzuri lakini siwezi kuwatumia wote kwa pamoja ila atacheza tu, mechi bado ni nyingi.”
No comments