Breaking News

SHOLO MWAMBA: DOGO JANJA ALINIHARIBIA


Sholo Mwamba.

MWAMBA wa Muziki wa Singeli, ‘Sholo Mwamba’ amedai kuwa, msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja ndiye aliyemharibia na kumfanya kujitoa katika menejimenti yake ya zamani baada ya kubaini kuwa na uhusiano na bosi wake.

Akipiga stori Over Ze Weekend, Sholo Mwambaanayekimbiza na ngoma kibao ikiwemo Geto alisema, ukiachilia mbali matatizo mengine ya kimaslahi na maendeleo ya muziki wake, moja ya mambo yaliyomfanya ajitoe kwenye menejimenti hiyo ni kitendo cha bosi wake kujihusisha kimapenzi na Dogo Janja.

Dogo Janja.

“Ukweli ni kwamba penzi la aliyekuwa bosi wangu na Dogo Janja ni moja ya sababu ya mie kujiengua kwenye menejiment, uhusiano wao wa kimapenzi umekuwa ukinichefua vibaya na kufanya muziki wangu kuzorota, maisha yangu hayaeleweki kifupi ni kama dogo ameniharibia,”alisema Sholo.


No comments