RUVU SHOOTING KUIKATIA RUFAA KAGERA SUGAR
Msemaji wa Ruvu Shooting amesema wamepeleka malalamiko yao kwa kamishina wa mchezo wao wa juzi kutokana na Kagera Sugar kumchezesha Adeyun Saleh ambaye hajamaliza mkataba wake na Stand United.
"Tunataka kucheza soka la haki, Adeyun, hajamaliza mkataba wake na Stand United, lakini wao wamemtumia kwenye mchezo baina yetu, hii ni makosa huyo kamishina atatupelekea sehemu sahihi, ili haki ipatikane," anasema.
Matokeo ya bao 1-1 ya juzi Jumapili yameiweka timu hiyo kwenye nafasi ya 14 wakiwa na pointi moja.
No comments