Breaking News

RONALDO ATESWA NA MABAO


Ronaldo anaonekana anataka kusahau mwanzo wake mbaya wa msimu wakati atakapoiongza Real Madrid katika kusaka rekodi ya kutwaa mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa katika mchezo wao wa leo Jumanne dhidi ya Borussia Dortmund.

Madrid, Hispania.Kucheza mechi mbili bila ya kufunga bao ni jambo la kawaida kwa wachezaji wengi, lakini kwa Cristiano Ronaldo hali hiyo ni ishara ya ukame.

Ronaldo anaonekana anataka kusahau mwanzo wake mbaya wa msimu wakati atakapoiongza Real Madrid katika kusaka rekodi ya kutwaa mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa katika mchezo wao wa leo Jumanne dhidi ya Borussia Dortmund.

Mreno huyo ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kuifikia rekodi ya Lionel Messi ya kutwaa mara tano taji la Ballon d'Or kutokana na mchango wake kwa Madrid kwa kutwaa ubingwa wa La Liga na Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.

Hata hivyo mwanzo mzuri wa Messi akiwa na Barcelona na uhamisho ghali wa Neymar wenye thamani ya dola 265 milioni kwenda Paris Saint-Germain mwezi uliopita vinamfanya Ronaldo kuwa katika ushindani mkali.

Watatu hao wametajwa katika orodha ya wachezaji walioingia katika kinyang’anyiro cha kuwani tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa Fifa 2017.

Ni Ronaldo nayeonekana kuanza msimu vibaya na kusababisha Real kuwa nyuma kwa pointi saba kwa Barca katika mbio za ubingwa wa La Liga.

Baada ya kufungiwa mechi tano kwa kumsukuma mwamuzi baada ya kupewa kadi nyekundu katika mchezo wa Spanish Super Cup.

Adhabu hiyo imekwisha vibaya kwa Ronaldo katika mchezo wa kwanza aliorejea uwanjani alishudia Real ikipoteza rekodi yake ya kushinda mechi 73 mfululizo baada ya kuchapwa 1-0 na Real Betis wiki iliyopita.

Ronaldo pia alitoka mtupu wakati Madrid ikipata ushindi wa tabu dhidi ya Alaves pamoja na kupiga mashuti 18 katika mechi mbili zilizopita.

 "Cristiano yupo tayari wakati wote. Wakati anaposhindwa kufunga niulizeni mimi kuhusu yeye," alisisitiza kocha wa Real, Zinedine Zidane.

"Anataka kufunga kama kawaida yake, lakini msimu ndiyo kwanza umeanza, mwisho atawashangaza watu kwa kile atakachokuwa amekifanya."


No comments