Breaking News

Kocha Omog awaweka wachezaji roho juu

KATIKA kikosi cha Simba habari kubwa ni kubadilishwa kwa safu ya ulinzi ambapo mpaka sasa wameshacheza mabeki sita; Juuko Murshid, Method Mwanjali, Ally Shomary, Mohammed Hussen ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni na Salim Mbonde.

Kocha wa timu hiyo, Joseph Omog, amesema katika kikosi chake hakuna mchezaji mwenye uhakika wa namba, isipokuwa atakayefanya vizuri akiwa mazoezini ndio atapata nafasi ya kucheza kwenye mechi.

Omog alisema: “Nimekuwa nikibadilisha mabeki kutokana na mechi inavyotaka. Huwa nawaangalia wapinzani na kuona nani acheze, ndio maana nimetumia mabeki wote sita na mpaka ligi itakapomalizika nitatumia zaidi ya hao.

“Siyo mabeki tu, bali nitakuwa nabadilisha wachezaji kulingana na uwezo wao mazoezini, lakini pia nitakuwa naangalia wapinzani wanacheza kwa aina gani, ili nijua nami niwatumie wachezaji wa aina ipi.”

Kwa sasa Simba ipo Tabora ilikojichimbia kwa muda kabla ya kwenda Shinyanga kucheza na Stand United mechi ya Ligi Kuu Bara. Juzi Jumapili ilicheza mechi ya kirafiki na Mirambo ambapo hazikufungana. Imetokea Mwanza ilitoka 2-2 na Mbao FC kwenye mechi ya ligi.

No comments