Mwigulu Nchemba Ataja Sababu za Masheikh wa Zanzibar Kushitakiwa Bara
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amefunguka na kusema kuwa mtu yoyote akifanya makosa ya nchi nzima atachukuliwa na kupelekwa sehemu yoyote ambapo mamlaka zinazofanya jambo hilo zitaona panafaa.
Mwingulu Nchemba amesema hayo jana wakati akijibu swali la Mbunge Dkt. Suleman ambaye alihoji uhalali wa baadhi ya Masheikh kuhamishwa kutoka Zanzibar na kuletwa Tanzania Bara kuhukumiwa katika mahakama za Tanzania bara na kusema ni kinyume na sheria.
"Mhe Spika spingani na muuliza swali kwenye upande wa vipengele vya sheria lakini naomba nimwambie tu kwamba kuna makosa ambayo 'specifically' siyo ya kijiografia mfano watu wakifanya makosa ya kung'oa michikichi Kigoma hilo unaweza kulitaja ni kosa la Kigoma, kama watu watang'oa karafuu Pemba ni kosa ambalo unaweza kusema la Pemba.
".... lakini yanapofanyika makosa ya nchi nzima Mtanzania yoyote au raia yoyote awe wa Tanzania au nje ya Tanzania atachukuliwa na taratibu za kufuata haki na sheria zitafanyika pale ambapo mamlaka inayofanya hatua hizo inaona ndipo panafaa"alisema Mwigulu Nchemba
No comments