Breaking News

MTIBWA SUGAR KUVAANA NA YANGA JUMAMOSI


Klabu ya Mtibwa Sugar kutoka Turiani mkoani Morogoro inataraji kutinga uwanjani siku ya Jumamosi  tarehe 30.09.2017  kucheza mchezo wa ligi kuu bara  namba 34 dhidi ya Young Africans utakaopigwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es laam.

Klabu ya Mtibwa  inayomilikiwa na kiwanda cha kuzalisha sukari bora nchini  Mtibwa Sugar ni klabu inayo ongoza msimamo wa ligi kuu bara hadi sasa kwa kwa kufanikisha kukusanya pointi 10 katika michezo 4 iliyocheza kwa upande wa Young Africans wao wanashika nafasi ya 6 baada ya kukusanya pointi 8 katika michezo 4 ya ligi kuu bara.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali kutokana na matokeo ya timu hizi mbili karibuni kuwa mazuri ila Mtibwa Sugarikionekana bora na kuongoza ligi kuu bara hadi mzunguko wa nne.

Kuelekea mchezo huo kikosi cha wana tam tam kimejichimbia mkoani Morogoro katika maskani yake Madizini Turiani kikiendelea na maandalizi ya mchezo huo wa Jumamosi.

Mchezo wa mwisho baina ya timu mbili zilitoka sare ya bila kufungana katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro  na Jumamosi zitakutana katika uwanja wa Uhuru .

RATIBA:

MCHEZO: Young Africans V Mtibwa Sugar

LEAGUE:  Vodacom Premier League

SIKU:         Jumamosi

TAREHE: 30.09.2017

UWANJA: Uhuru Stadium

No comments