MRADI WA BOMBA TANGA WANANCHI WARUBUNIWA NA MATAPELI
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amewaonya wakazi wa jiji la Tanga kutokubali kurubuniwa na genge la matapeli linalotoa matangazo ya kazi na kuwalipisha watu fedha kwa ahadi ya kuwapatia ajira katika mradi wa bomba la mafuta linalojengwa kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza kwenye baraza la madiwani wa jiji hilo kufuatia taarifa za kuzuka kwa magenge ya utapeli yaliyojipachika uwakala wa kusimamia mchakato wa ajira kutoka katika mradi huo.
Amesema ajira za Serikali zinatangazwa kupitia utaratibu wa wazi ambao upo kisheria bila ya kupitia kwa uwakala.
Kwa upande wake meya wa jiji la Tanga Mhina Mustafa (Selebos ) amesema halmashauri imekamilisha upimaji wa viwanja 4000 katika maeneo ya amboni ambavyo vitatangzwa hivi karibuni na kuwataka wananchi kujitokeza kuomba.
Aidha amewaonya wananchi wanaonunua viwanja kiholela na kujenga bila kibali cha jiji kuacha mara moja ili kuepuka kubomolewa nyumba zao.
Katika hatua nyingine baraza limewasimamisha kushiriki vikao vitatu madiwani watano kwa kosa la utovu wa nidhamu.
No comments