Breaking News

MAN UNITED YAMNYEMELEA PAULO DYBALA WA JUVENTUS MAMBO YAKO HIVI

 

MANCHESTER UNITED wanaandaa ofay a paundi milioni 155 kwa ajili ya kumnyakua nyota wa Juventus Paulo Dybala.

Mshambuliaji huyo raia wa Argentina alitupia mabao mawili kwenye ushindi wa 4-0 ambao mabingwa watetezi hao waliupata dhidi ya Torino mwishoni mwa wiki huku gazeti la Sunday Mirror la nchini Uingereza likiripoti kuwa mabosi wa United wanajiandaa kuchuana vikali na Barcelona

Juventus wamesisistiza kuwa Dybala mwenye umri wa miaka 23 hana kipengere cha ofa maalum ya kuuzwa kwenye mkataba wake na ofa yoyote ambayo itazidi ile ya Paul Pogba basi watakubaliana nayo

Hata hivyo bosi wa Juventus, Giuseppe Marotta amesema kuwa hatamzuia nyota huyo kuondoka

Dybala amefunga magoli 12 kwenye mechi nane azlizoichezea Juventus msimu huu huku akiwa anaendelea kuimarika

No comments