Breaking News

Nyota wa Serengeti Boys ajiweka sokoni

Kinda huyo amesema kuwa licha ya kuachwa na timu hiyo ya Taifa, lakini bado uwezo wake ni uleule hivyo timu yoyote yenye kuhitaji huduma yake anaikaribisha.

Mwanza. Aliyekuwa mchezaji wa Serengeti boys,Cyprian Benedicto amesema  ameamua kujiingiza kwenye michuano ya Ndondo Cup ili wadau na timu zinazoshiriki ligi za juu waweze kumuona uwezo wake.

Kinda huyo amesema kuwa licha ya kuachwa na timu hiyo ya Taifa, lakini bado uwezo wake ni uleule hivyo timu yoyote yenye kuhitaji huduma yake anaikaribisha.

"Nimeona nisilale tu nyumbani wakati nina kipaji changu, kwahiyo ndio maana nimekuja hapa kucheza Ndondo ili watu na timu wanione" amesema Kinda huyo.

Hata hivyo kiungo huyo mshambuliaji anayekipiga kwenye timu ya Bwiru Star ameibuka mchezaji bora kwenye mechi ya Ndondo cup dhidi ya Phantom na kujipatia sh 30,000 licha ya timu yake kulala kwa  mabao 2-0.

No comments