Breaking News

KUN AGUERO ANUSURIKA KIFO

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Sergio Kun Aguero amepata ajali mbaya ya gari iliyopelekea kuvunjika mbavu mjini Amsterdam nchini Uholanzi ambako alikwenda kwa ajili ya tamasha la muziki.

Taarifa zinasema Aguero alikuwa njiani kuelekea uwanja wa ndege wa Amsterdam na ndipo Taxi hiyo ilipoteza uelekeo barabarani na kugonga nguzo ya taa iliyokuwa pembeni mwa barabara.


Tamasha alilokwenda Aguero ni la msanii aliyetambulika kama Maluma na polisi wamesema seat belt aliyovaa ilimsaidia kumuokoa lakini laa sivyo ingekuwa habari kubwa zaidi.

Inaonekana wakati gari linagonga nguzo belt aliyovaa Aguero ilisaidia kumzuia asisogee mbele na kama asingevaa angesogezwa mbele zaidi ya gari jambo ambalo lingemsababishia tatizo kubwa sana.

Aguero ambaye ameifungia Manchester City mabao 7 katika mashindano yote msimu huu atakosa mechi dhidi ya Chelsea mwishoni mwa wiki na pia atakosa mchezo kati ya Argentina.



No comments