KATIBU MKUU WA CHADEMA , DR. VICENT MASHINJI AKATAA WITO WA POLISI
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema hawezi kwenda kuripoti Polisi kama alivyotakiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto kwa kuwa hakuambiwa siku maalumu ya kwenda.
Kamanda Muroto amemtaka Dk Mashinji afike ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya jinai mkoani Dodoma au ofisi kama hiyo iliyopo Kituo cha Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ili kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kuhusu tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
“Nina taarifa za kuitwa Polisi, lakini haziko ‘specific’. Ni wakati wowote naweza kwenda? na hawajasema nikaripoti wapi. Kwa hiyo, wakinihitaji watakuja kuniambia,” amesema Dk Mashinji akizungumza na Mwananchi.
Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mchana alipokuwa akielekea nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.
Kwa sasa Lissu anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi, Kenya.
No comments