HIMID MAO AWAZUNGUMZIA WACHEZAJI WA AZAM WALIOHAMIA SIMBA
KIUNGO wa Azam, Himid Mao amesema kuwa wapinzani wao simba wako vizuri kutokana na kuwachukua majembe yao wakiwemo Aishi Manula na John Bocco.
Himid ameimbia shaffidauda.co.tz
kuwa wapinzani wao Simba wapo vizuri ikizingatiwa kwamba wameweza kuwachukua nyota kadhaa ambao walichangia maendeleo ya timu hiyo akiwemo Boco.
“Simba wapo vizuri kwa msimu huu kwa usajili wao hasa kwa kuwachukua wachezaji wetu ambao walikua muhimu hapa, ila naamini tutashinda licha ya kuwa ni mechi ngumu,”-Himid nahodha Azam FC.
Himid ambae ni rafiki mkubwa wa John Bocco amesema Simba wamewasajili Aishi Manula na Bocco ambao anaona watawasaidia.
Himid kwa mara ya kwanza atakutana na waliokuwa wachezaji wenzake walio hama Azam kwenda Simba.
No comments