Breaking News

CHELSEA KUFUNGIWA KUFANYA USAJILI NA FIFA


Kwa mara ya 8 klabu ya Chelsea imeingia matatani tena na shirikisho la soka duniani FIFA kutokana na kukiuka sheria za usajili wa wachezaji vijana, na sasa FIFA wameanza rasmi uchunguzi wao.

Haijafahamika wazi ni wapi Chelsea wameonekana kukiuka sheria za usajili kwa wachezaji vijana lakini taarifa kutoka FIFA zimethibitisha kwamba wanaanza kufanya uchunguzi kuhusiana na klabu hiyo.

Kama unakumbuka hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Chelsea kukumbwa na kesi za namna hii kwani mwaka 2009 tu walifungiwa kufanya usajili baada ya kukiuka sheria lakini walikata rufaa na kushinda kesi hiyo.

Mwaka jana pia Chelsea wakaingia matatizoni na FIFA kuhusiana na wachezaji vijana baada ya kugundulika kumtumia Bertand Troure huku wakijua umri wake kutumiaka katika baadhi ya mechi ulikuwa bado.

Msemaji wa FIFA alipoulizwa kuhusiana na hili la kuichunguza Chelsea amekiri kwamba upelelezi unaendelea dhidi ya klabu hiyo lakini akakataa kuweka wazi kwamba nini haswa Chelsea wamefanya.

Matukio kama haya ya kukiuka sheria za usajili yamevigharimu vilabu vingi ambapo kama unafahamu klabu ya Athletico Madrid imekula pini kuhusu kufanya usajili kutokana na kukiuka sheria ya usajili.

Haijafahamika bado ni adhabu gani Chelsea watapewa wakikutwa na hatia lakini kosa walilofanya wao sio kubwa kama la Athletico Madrid na ni wazi hawatapewa adhabu kubwa.


No comments