Bocco: Nipeni muda, nitafunga zaidi
Straika wa Simba, John Bocco amewaomba mashabiki wa timu kumvumilia kwa muda kabla ya kuonyesha makeke yake aliyokuwa nayo Azam.
Bocco aliyeifungia Simba bao lake la kwanza kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga amesema anahitaji muda zaidi kwa ajili ya kuonyesha makali yake aliyokuwa nayo Azam.
“Kwanza kwa wale ambao wanasema nimeshuka kiwango pole yao kwa sababu bado na uwezo Mkubwa, Lakini nahitaji muda zaidi hapa Simba kabla ya kuonyesha makali yangu ambayo nilikuwa nayo Azam,” alisema Bocco ambaye bao lake dhidi ya Mwadui alilitoa zawadi kwa mama yake.
Mchezaji huo wa Zamani Wa Azam FC alisema anaamini akipewa nafasi mara kwa mara katika kikosi cha kwanza ataweza kufunga mabao mengi.
No comments