Breaking News

BAD NEWS; AJARI YASABABISHA VIFO ZAIDI YA WATU 35 MUSOMA

Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara likiwa limeharibika vibaya baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba,Mjini Musoma mchana huu.

Watu zaidi ya 35 wamepoteza maisha papo hapo na wengine zaidi ya 86 kujeruhiwa vibaya. Kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio hivi sasa,inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi,liliisukuma ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni.

Hali iliyoipelekea basi hilo kuamini kuwa itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.Ndani ya gari hiyo ndogo kulikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa.Picha


No comments