Breaking News

Watoto wa Wenger kufungua dimba la EPL

Utamu wa Ligi Kuu ya England unarejea kuanzia leo ambapo watoto wa mzee Wenger, Timu ya Arsenal itafungua dimba hilo kwa kuoneshana ubabe na Leicester City.

Kuelekea mchezo huo unaopigwa Emirates, Arsenal imejiweka sawa kuendeleza rekodi yake ya kuinyanyasa Leicester City katika ligi hiyo, huku ikitafuta nafasi ya kurekebisha makosa katika mechi za fungua dimba ambapo katika mechi 7, imeshinda mechi moja pekee.

Arsenal wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kutwaa ubingwa wa ngao jamii dhidi ya mabingwa wa EPL Chelsea FC lakini inamkosa mshambuliaji wake tegemeo Alexis Sanchez ambaye ni majeruhi.

Baada ya mechi hiyo ya ufunguzi inayopigwa saa 3:45 usiku wa leo , mechi nyingine saba zinapigwa kesho Jumamosi kama ifuatavyo:-

Watford Vs Liverpool

Chelsea Vs Burnley

Crystal Palace Vs Huddersfield

Everton Vs Stoke City

Southampton Vs Swansea City

West Brom Vs Bounermouth

Brighton Vs Man City

Ligi hiyo itaendelea tena Jumapili ambapo Man United itakuwa mwenyeji wa West Ham wakati Tottenham ikianzia ugenini dhidi ya Newcastle United

No comments