Wakenya waanza kumiminika Tanzania
Hofu imetawala kina kona nchini humo wakati siku za uchaguzi mkuu zikikaribia
Joto la uchaguzi wa nchini Kenya limezidi kupamba moto kufuatia
idadi ya Wakenya wanaoingia Tanzania kwa kuhofia fujo ikizidi kuongezeka.
Mwananchi ilikuwa katika vijiji vilivyo jirani na mpaka wa
Horohoro mkoani Tanga na kukuta idadi ya wanaovuka kutoka Kenya
kuingia Tanzania kuwa kubwa ikilinganishwa na siku ambazo si za
uchaguzi.
Mwanakombo Ali ambaye ni Mkazi wa Vanga nchini Kenya amesema
amelazimika kuondoka kutokana na hofu kwamba
huenda siku ya uchaguzi ikatokea vurugu.
“Mimi na watoto wangu watatu tumekuja hapa Duga Maforoni kwa baba
yangu,huku ndiko nyumbani kwetu na Vanga ni kwa mume wangu kwani hivyo
nimeona nising’anganie kukaa mahala ambapo tunaweza kuuawa ikitokea
vurugu”amesema Mwanakombo.
Salehe Mohamed amesema katika kijiji cha
Mwakijembe wilayani Mkinga mkoani Tanga kuwa yeye ni mkazi wa Mombasa
nchini Kenya na alikuwa amejiandikisha kupiga kura lakini kutokana na
hofu ya kutokea vurugu ameamua kuondoka yeye na familia yake ili
kuokoa maisha.
“Tutakaa hapa hadi uchaguzi utakapofanyika na kutajwa mshindi kwani
hali si shwari kwa sasa hivi akishinda Uhuru kutatokea vurugu na hata
akishinda Odinga kutatokea vurugu tu”amesema Salehe.
Katika mapaka wa Kenya na Tanzania,Mwananchi ilishuhudia abiria
wanaoingia Tanzania kupitia mabasi ni kubwa kuliko wanaokwenda Kenya
ambapo wengi wao ni raia wa wa Kiasia na kutoka nchi za Ulaya.
Ofisa mmoja idara ya uhamiaji katika ofisi ya Horohoro ambaye hakutaka
jina lake litajwe amesema kumekuwa na idadi kubwa ya abira wanaopita
katika mpaka huo wakitokea nchini Kenya kuingia Tanzania na sababu ni
kutokana na uchaguzi
Post Comment
No comments