Zitto Kabwe amtete Halima Mdee
Kiongozi wa Chama Cha Act-Wazalendo amesema kuwa Kukamatwa kwa Mbunge wa kawe Halima Mdee ni matumizi mabaya ya Madaraka.
"Amri ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni kumkamata Mbunge Halima James Mdee ni mwendelezo wa matumizi mabaya ya madaraka. Inasikitisha Sana kuona viongozi vijana wanafanya mambo ya hovyo Kabisa. Sheria ya DC kumweka mtu kizuizini Ina masharti yake na haihusiani kabisa na yanayoitwa makosa ya ndugu Halima Mdee."
Tunapaswa kulaani Kwa nguvu Sana mambo haya kwani yataota mizizi na kuathiri watu wengi zaidi
No comments