Walimu wastaafu waiomba Serikali iharakishe Malipo yao
BAADHI ya walimu wastaafu wilayani mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali ya awamu ya tano kuharakisha malipo ya mafao yao kwa ajili ya kuwapunguzia ukali wa maisha kipindi cha kustaafu.
Miongoni mwa changamoto zinazowakabili walimu hao ni pamoja na kutoonekana kwa mafaili ambayo ndiyo hutunza kumbukumbu zao pamoja na wengine kupewa kauli mbaya na viongozi wa halmashauri wakati wa kufatilia stahiki zao.
Mwenyekiti wa Chama cha Walimu wilaya ya Mufindi amesema changamoto hizo zimedumu kwa muda mrefu huku kubwa likiwa ni kutoonekana kwa mafaili yao, huku baadhi yao wakiambiwa ni watumishi hewa hali inayo wapa hofu kubwa wakati wakikaribia kustaafu.
Kwa upande wao wastaafu hao watarajiwa akiwamo Victoria Baston na Julius Matege wamesema changamoto wanazokumbana nazo wakati wa kufuatilia stahiki zao ni serikali kutowalipa nauli za kuwarudisha majumbani mara baada ya kustaafu kama wanavyoeleza.
No comments