Tetesi za usajili barani Ulaya
Inasemekana klabu ya Chelsea iko mbioni kukamilisha mlinzi kitasa wa klabu ya As Roma Toni Rudiger kwa uhamisho ambao utaigharimu klabu ya Chelsea zaidi ya €33m, uhamisho huu umekuja baada ya Conte kuona ugumu katika kununua wachezaji wakubwa.
Klabu ya Arsenal inajiandaa kuvunja rekodi ya usajili ndani ya klabu hiyo kwani wanajiandaa kutuma ofa ya kiasi cha €50m kwenda katika klabu ya Lyon ili kumnunua mshambuliaji Alexandre Lacazette.
Tayari Jermain Defoe amesaini wino katika klabu ya Afc Bournamouth ambapo dili hilo limeigharimu klabu hiyo kiasi cha euro 20m kutoka klabu ya Sunderland.
Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Pedro Rodriguez amekiri kwamba kama Diego Costa ataondoka litakuwa pigo kubwa sana kwao, tayari kocha Antonio Conte amesema hana mpango na Costa katika msimu ujao wa ligi.
Baada ya kupoteza sana nafasi chini ya kocha Pep Gurdiola, mshambuliaji wa Man City Kelechi Iheanacho anaweza kutimkia katika klabu ya Southampton kwa dau la €25m.
Baada ya tetesi kuzagaa kwamba klabu ya Fc Barcelona inamtaka Ander Herrera, sasa klabu ya Manchester United imeibuka na kutangaza kwamba kiungo huyo hauzwi kwa dau lolote na hataondoka United.
No comments