SONGWE:MKUU WA WILAYA ATOA AMRI KWA VIJANA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA MGAMBO KWA LAZIMA
VIJANA katika kata za kata za Saza na Mbangala Wilayani Songwe Mkoani Songwe wameyakimbia makazi yao na kwenda kuishi porini wakikwepa amri ya Mkuu wa wilaya ya songwe, inayowataka vijana wote wa kata hiyo kuanza mafunzo ya mgambo kwa nguvu, wakidai hawakushirikishwa .
Hatua ya kukimbia makazi yao na kuziacha familia zao na kwenda kuishi porini kwa vijana hao kunadaiwa kumetokea baada ya Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samuel Jeremiah kutoa amri ya kuwataka vijana wote wenye umri wa miaka kati ya 18 na 35, kuanza mafunzo ya mgambo kwa nguvu, hali ambayo imesababisha maisha ya vijana hao pamoja na familia zao kuwa mashakani.
Vijana hao ambao ni wachimbaji wadogo wa madini na kipato chao kikiwa kinategemea uchimbaji wa madini ili kujikimu kimaisha kumesababisha athari kubwa katika shughuli za kiuchumi na kijamii, hivyo kuathiri maisha ya wakazi wote wa kata hizo.
Channel ten ikapiga hodi hadi ofisi za Mkuu wa Wilay aya Songwe Samuel Jeremih akasema suala la mafunzo ya mgambo siyo la hiari kwa sababau ni kwaajili ya usalama wa Taifa .
No comments