NDUGU WA NIYONZIMA WAWASILI KWA MAFUNGU MWANZA
Haruna Niyonzima.
KIUNGO anayemaliza mkataba Yanga, Haruna Niyonzima ni raia wa Rwanda, sasa kikosi cha timu yake ya Taifa leo kinacheza dhidi ya Taifa Stars bila yeye kuwemo, timu hiyo imewasili nchini kwa mafungu.
Hata hivyo, Niyonzima hayumo katika kikosi hicho kwani ni kile kinachoshiriki kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwaWachezaji wa Ndani (Chan). Niyonzima bado hajafanyiwa uhamisho Yanga na anahesabika anacheza nje ya nchi yake.
Rwanda maarufu kama Amavubi kikosi chake kilianza kuwasili kwa mafungu ambapo kundi la kwanza liliwasili saa 2:00 asubuhi huku kundi jingine likiwasili saa 5:00 asubuhi.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema kuwa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ambao ndiyo waandaji waChan, waliwaambia kuwa Rwanda itaingia nchini kwa mafungu.
“Hii mechi inasimamiwa na Caf, sasa Caf wao ndiyo waliotuambia Rwanda wataingia hapa nchini kwa mafungu kutokana na kukosa ndege ya pamoja hivyo ndivyo ilivyo,” alisema Lucas.
Lucas alisisitiza kuwa, Caf pia inatambua kwamba mchezo huo ni lazima uchezwe kwenye Uwanja wa CCM Kirumba licha ya Rwanda kuchelewa na maandalizi yote yamekamilika.
Tayari mwamuzi Alier Michael James wa Sudan Kusini atakayechezesha mchezo huo leo ameshafika jijini Mwanza na wasaidizi wake.
No comments