JUUKO AIKACHA SIMBA SC
Beki wa Simba, Juuko Murshid raia wa Uganda.
BEKI wa Simba, Juuko Murshid raia wa Ugandayupo mbioni kutua kuichezea Orlando Piratesya Afrika Kusini.
Mganda huyo, bado ni mchezaji halali wa Simba mwenye mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya kuichezea timu iliyoweka kambi yake nchiniAfrika Kusini kujiandaa na msimu ujao.
Beki huyo inaelezwa hadi hivi sasa hajajiunga kwenye kambi ya timu hiyo ambapo inadaiwa hana mpango wa kurejea Msimbazi.
Juuko anayeichezea timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ anahusishwa kutua Orlando Pirates na mtandao mmoja mkubwa wa nchini huko.
Mtandao huo unaeleza kuwa, wakati beki huyo akigomea kambi ya Simba iliyoweka kambi yake Afrika Kusini yeye anajifua kwa nguvu zote na timu yake ya taifa kwa ajili ya kujiweka sawa akijiandaa kutimkia Sauzi.
Beki huyo wa zamani wa Bunamwaya ‘Vipers’ na SC Victoria University anajinoa na The Craneskatika kikosi kinachojiandaa na fainali za kufuzuCHAN 2018 dhidi ya Sudan Kusini.

No comments