Breaking News

HAMISSA MOBETO AMUANIKA BABA KIJACHO WAKE

Muuza nyago kwenye video za wasanii, Hamissa Mobeto.

Muuza nyago kwenye video za wasanii, Hamissa Mobeto anayehisiwa kuwa ni mama kijacho, kutokana na baadhi ya picha zake za hivi karibuni zikimuonyesha akiwa ameshiba yaani kitumbo ndiii!!!

Huku Wabongo wakiwa bado wanajiuliza swali la ni nani hasa baba kijacho wa kitumbo hicho, wengine wakienda mbali zaidi na kuhisi labda huenda hicho kibendi ni cha mmoja wa wasanii waliowahi kujivinjari naye au ni cha baba wa mtoto wake wa kwanza!

Sasa jana kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Mobeto kaliamsha dude baada ya kuposti picha yake na kuandika maelezo yafuatayo; Mama daa…Mama dee…Mama dii…Mama doo… Mama duu… ambapo mashabiki wakafananisha maelezo hayo na hisia zao za muda mrefu kuwa kibendi hicho ni cha yuleyule msanii wa bongo fleva aliyekuwa akihisiwa.

No comments