CHADEMA NDIO BASI TENA PIGO JINGINE HILI HAPA
Madiwani watatu wa Jimbo la HAI ,Kilimanjaro watangaza kujiunga na CCM wakitokea CHADEMA.
1. Bw. Kiwili wa kata ya Weruweru,
2. Bw. Kimaro wa Machame Magharibi na
3. Evarist Kimathi wa Mnadani.
BAADA YA MADIWANI, WATAKAOFUATA NI WABUNGE....
Madiwani watatu wa CHADEMA katika jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro wamejiuzulu nafasi zao na kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi CCM, kwa maelezo kuwa wanamuunga mkono Rais Magufuli.
Madiwani hao ni Bw. Kiwili wa kata ya Weruweru, Bw. Kimaro wa Machame Magharibi ambaye pia alikuwa ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai na Evarist Kimathi wa kata ya Mnadani.
Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kupokelewa na katibu wa itikadi na uenezi wa CCM taifa, Humphrey Polepole uliofanyika katika ofisi za CCM mkoa wa Kilimanjaro, madiwani hao wamesema kuwa wameridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli na hivyo wameona ni vema kuungana naye kuiletea maendeleo Tanzania wakiwa CCM.
Sababu nyingine iliyotajwa na madiwani hao ni migogoro ndani ya baraza la madiwani wanayodai kuwa inasababishwa na uongozi wa juu wa CHADEMA unaofanya chama kuwa ni mali ya mtu mmoja na kuminya demokrasia ndani ya chama.
Pia wamesema sababu nyingine ni kutelekezwa na mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ndiye mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe, wakidai kuwa tangu uchaguzi umemalizika, mbunge huyo hajaonekana jimboni na kuwafanya wao kama madiwani kushindwa kumuwajibisha pale wanapoona jambo fulani la maendeleo halijafanyika.
Kwa upande wake Polepole amewaonya watu ndani ya chama wanachotoka madiwani hao kutowadhuru wanachama hao wapya wa CCM huku akisisitiza kuwa lengo la chama hicho ni kuhakikisha Dkt. Magufuli anashinda kwa asilimia zaidi ya 75 katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

No comments