Yanga: Uhakika Mbaraka Yusuph Anatua Jangwani
YANGA imesema ina uhakika wa kumsajili mshambuliaji wa Kagera Sugar, Mbaraka Yusuph na imedharau taarifa za Azam FC kumuwania mchezaji huyo.
Kuongeza uhakika wa jambo hilo, Kagera Sugar imedai ilimtaka Mbaraka ajiunge na Yanga ambayo inamuhitaji kwa udi na uvumba na siyo timu nyingine hivyo wao wanajua anaenda hapo. Habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga, zinasema tayari mchezaji huyo ameshamalizana na timu hiyo na kilichobakia ni kutangazwa tu.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Meneja wa Kagera Sugar, Mohammed Hussein alisema: “Tulimzuia Mbaraka asiende Azam kwani ndoto zake ni kucheza michuano ya kimataifa mwakani.
“Tunachojua ni kwamba yeye anazungumza na Yanga na mambo yanaenda vizuri, Yanga inacheza Klabu Bingwa Afrika mwakani, hivyo ni sehemu sahihi kwa Mbaraka.
“Hatukupenda aende Azam kwa sababu tuliona atakuwa hajazitendea haki ndoto zake hizo na kuziacha zikapotea hivi hivi, huyu ni mali ya Yanga.”
Hata hivyo mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye aliomba kutotajwa jina lake gazetini ameliambia Championi Jumamosi kuwa tayari mchezaji huyo wameshamalizana naye na kilichobakia ni kutangazwa tu.
“Tunawashangaa na kudharau taarifa za Mbaraka kwenda Azam, ukweli ni kwamba mchezaji huyo ni mali yetu mpaka sasa tayari tumeshamalizana naye na tumempatia mkataba wa miaka miwili,” alisema bosi huyo.
Mwenyewe Mbaraka alidai: “Akili yangu nimeielekeza kwa timu ya taifa naomba niulize baada ya mechi yetu ya kesho (leo dhidi ya Lesotho) kwani nitapoteza umakini
No comments