Breaking News

Yanga kuibeba Tanzania kesho


Wachezaji wa Yanga
Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Yanga SC wanatarajia kushuka dimbani kesho kutupa kete yao ya pili kwenye michuano ya Sportpesa Super Cup dhidi ya AFC Leopards ya Kenya huku macho ya watanzania yakiwa kwa timu hiyo kuona kama itaweza kuleta ubingwa.

Timu ya Yanga ndiyo timu pekee inayoiwakilisha nchi ya Tanzania katika mashindano hayo baada ya Mabingwa wa Kombe la Shirikisho  Simba SC, Singida United na Jang'ombe ya Zanzibar kutolewa mapema katika hatua ya robo fainali ya michuano yenye mvuto wa aina yake.

Aidha siku ya kesho kutakuwa na mechi nyingine tofauti na Yanga ambayo itawakutanisha Gor Mahia dhidi ya Nakuru All Stars zote kutokea nchi ya Kenya katika hatua ya nusu fainali.

Katika mechi ya kesho timu itakayofanikiwa kumfunga mwenzake basi itakuwa imejikatia tiketi ya moja kwa moja kuingia katika fainali ya michuano ya Sportpesa Super Cup 2017 kuwania kitita cha Dola za kimarekani 30,000 sawa na Milioni 62 pesa ya kitanzania.

No comments