WANACCM: TUNABURUZWA NA RAIS MAGUFULI. WAPINGA UTEUZI WA MGHIRA..!!!
Rais kuteua wakuu wa mikoa toka vyama vya upinzani alipaswa kupata baraka za chama. Na ikibidi hata kubadilisha vifungu vya katiba ya ccm.
Nafasi ambazo rais huteua kwa matakwa yake bila ya kutungwa na katiba ya chama chake ni zile nafasi kumi za ubunge. Lakini kamwe siyo ukuu wa mikoa na wilaya. Hawa ni watekelezaji wa ilani ya chama kwa mujibu wa katiba ya ccm. Hivyo wanapaswa kuwa wafuasi ama wanazi wa ccm.
Huyu rais hana uchungu na chama na ni kwasababu hajawahi kukitumikia chama na hivyo hajui machungu ya kujenga chama. Kuna kila sababu ya kumpinga kwa nguvu zetu zote tutakapokutana ktk vikao vijavyo.
Haya yanaelezwa kwa uchungu sana na wanaccm, wazee kwa vijana wa sehemu mbalimbali nilikotembelea ili kupata maoni yao kufuatia uteuzi wa m/kiti wa chama cha ACT kuwa mkuu wa mkoa wa kilimanjaro
No comments