Breaking News

UMESEMA SABABU YA PENALTI NDIYO MAANA AGYEI ATAACHWA? UMEBUGI, SABABU SAHIHI HII HAPA...

Kipa Daniel Agyei sasa ameingia kwenye kapu la wanalotakiwa kuachwa Simba.

Mjadala wa Agyei raia wa Ghana abaki au aende umeanza siku tano zilizopita baada ya kamati ya ufundi ya Simba kukutana.

Imeelezwa, Simba kama itamnasa Aishi Manula basi itakuwa ni njia moja kwa Agyei kwa kuwa ingependa nafasi yake itumike kwa mchezaji mwingine.

"Mfano kama nafasi yake ikitumika kwa mchezaji wa ndani kunakuwa na faida kubwa. Kuna makipa wengi na hasa kama akipatikana Aishi Manula, basi ujue safari imemkuta Agyei," kilieleza chanzo.

Kuhusiana na suala la kukosa penalti katika michuano ya SportPesa kuonekana ndiyo sababu, chanzo kimefafanua:

"Suala la Agyei lipo mezani na lilikuwa likijadiliwa kwa misingi ya kitaalamu. Timu kama Simba ni kubwa, haiwezi kumuacha mchezaji sababu ya kukosa penalti.

"Wanaosema hivyo ni masuala ya kufikirika lakini sisi tunaangalia tifauti na suala hapa ni kipa wa nyumbani mwenye uwezo mzuri ili nafasi ya Agyei itumike kwa ajili ya wachezaji wengine wa ndani."

Agyei ametokea Medeama ya Ghana na kujiunga na Simba katikati ya msimu baada ya uongozi kuamua kipa Vicent Angban raia Ivory Coast kutupiwa virago baada ya kucheza nusu msimu akionyesha kiwango kizuri lakini akaboronga mechi mbili za mwisho.

No comments