Breaking News

Tunaotaka kuwa Viongozi bora tunajaribu kujinasibisha na Nyerere” – Makamba

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba amesema Kongamano la Mazingira lililofanyika Butiama ni kwa sababu Mwalimu Nyerere ni mfano wa kuigwa ambaye kila mmoja anatamani kumuiga katika yale aliyoyafanya.

Akizungumza katika Kongamano hilo lililofayika katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Mwitongo, Butiama Makambaamesema: “Katika mambo yote makubwa ya nchi: Umoja, Amani, Utulivu, Maadili mara nyingi rejea huwa ni Mwalim Nyerere. Na sisi wote ambao tunataka kuwa Viongozi bora tunajaribu sana kujinasibisha na Nyerere.”

Aidha, Waziri Makamba amesema moja ya sababu za kulipeleka Butiama Kongamano hilo ambako ni nyumbani kwa Hayati Baba wa Taifa ni kuuenzi mchango wa Mwalim Nyerere katika kutunza na kuhifadhi mazingira.

“…sisi ambao tunashughulika na mazingira, kutokana na changamoto kubwa ambayo tunaipata katika kusukuma ujumbe wa hifadhi ya mazingira, na sisi tumeamua tutumie sauti ya Mwalimu, tutumie kifua cha Mwalimu, tutumie mabega ya Mwalimu. Na hakuna sehemu nzuri ya kuanza hiyo harakati kama mahala alipozaliwa, mahala alipokulia na mahala alipozikwa, lakini pia mahala ambapo kazi ya mikono yake ya utunzaji na hifadhi ya mazingira inaonekana nayo ni Butiama.”– January Makamba

No comments