Breaking News

TETESI ZA USAJILI LEO JUNE 21. 2017




Barcelona KUFANYA USAJILI WA REKODI KWA DEMBELE

Barcelona wanataka kufanya uhamisho wa kuvunja rekodi kwa kumsajili nyota wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, kwa mujibu wa  Bild .

Mkurugenzi wa michez Robert Fernandez ni shabiki mkubwa wa mshambuliaji huyo wa BVB mwenye mkataba hadi 2021. Uhamisho huo utakuwa mauzo makubwa katika historia ya Bundesliga kwani utazidi euro milioni 75 Manchester City walizolipa kwa ajili ya Kevin De Bruyne 2015.



JUVENTUS YAMWANIA NEVES

Juventus imeungana na Liverpool na Chelsea katika mbio za kumfukuzia nyota wa Porto Ruben Neves, Mirror limeripoti.



MAN UTD HUENDA ISIMSAJILI RONALDO

Manchester United wanasita-sita kumsajili Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid, kwa mujibu wa  Daily Express .

Ronaldo inaaminika anatamani kuondoka Real Madrid, lakini Jose Mourinho anaogopa kuingia kwenye mbio hizo za kumsajili. United wanahofu ni hila za Ronaldo tu kutaka kupewa dili nono zaidi Madrid na hawataki kutumia muda kufanya mazungumzo na mchezaji ambaye hawatamsajili.



MAN CITY HAWANA MPANGO NA AUBAMEYANG

Manchester City hawajaandaa dau la paundi milioni 60 kwa ajili ya Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang kama tetesi zinavyodai, limeripoti  BBC .



OXLADE-CHAMBERLAIN KWENYE RADA UINGEREZA

Kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain yupo kwenye rada za Chelsea, Liverpool na Manchester City msimu wa majira ya joto, kwa mujibu wa Sky Sports.  



PEPE AMTAKA RONALDO KUTUA PSG

Pepe amemtaka Cristiano Ronaldo kuungana naye PSG baada ya mshambuliaji huyo kuonyesha nia ya kutaka kuondoka Real Madrid, kwa mujibu wa  El Transistor .




MAN UTD INATAKA KUMSAJILI SEMEDO

Manchester United wanaandaa upya ofa wakitaka kumsajili mchezaji wa Benfica Nelson Semedo baada ya kumsajili Victor Lindelof ambaye waliwahi kuwa kwenye timu moja, kwa mujibu wa  O Jogo .



LYON WATARAJIA KUMSAJILI TRAORE

Lyon ni miongoni mwa timu zinazopambana kukamilisha dili la paundi milioni 16.6 kumsajili Bertrand Traore kutoka Chelsea, kwa mujibu wa Evening Standard .



MATHIEU AKARIBIA KUTUA SPORTING

Beki wa Barcelona Jeremy Mathieu amesafiri hadi Ureno kukamililisha uhamisho kujiunga na Sporting Lisbon, kwa mujibu wa  A Bola .



BAYERN YAMFUKUZIA WALKER

Bayern Munich inataka kumsajili Kylie Walker kutoka Tottenham Hotspur, kwa mujibu wa  T he Sun .

Ada ya Muingereza huyo inakadiriwa kuwa paundi milioni 45.


ASANO AKATALIWA KUREJEA ARSENAL

Takuma Asano atabaki kwa mkopo Stuttgard akitokea Arsenal kwa msimu mmoja zaidi, limeripoti jarida za Ujerumani  Bild .



ARSENAL IPO TAYARI KUTOA €30M KUMSAJILI TURAN

Arsenal wanaandaa dau la euro milioni 30 kumsajili Arda Turan kutoka Barcelona, kwa mujibu wa ripoti kutoka  Uturuki na Spain .


MBAPPE AMEICHAGUA MADRID

Kylian Mbappe ameiweka wazi Monaco kuwa anataka kujiunga na Real Madrid majira ya joto, limeripoti jarida la  Marca .

JUVE & ARSENAL ZAMWANIA ASENSIO

Marco Asensio anafikiria kuondoka Real Madrid uhamisho wa majira ya joto, Juventus na Arsenal zinavutiwa na huduma yake, limeripoti Diario Gol.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 alijiunga na Madrid akitokea Mallorca miaka mitatu iliyopita na ameonyesha mwanga wa kufanikiwa, lakini anataka muda zaidi wa kucheza. 

BVB WANAMTAKA NYOTA HUYO WA BARCA

Borussia Dortmund wanajipanga kumsajili mchezaji wa Barcelona Lee Seung-Woo, Bild  limesema.

UTD & BAYERN ZAMFUATILIA DEMBELE

Manchester United na Bayern Munich watamfuatilia kinda wa Celtic mwenye umri wa miaka 14 Karamoko Dembele katika shindano la vijana majira ya joto, The Sun limeripoti.

Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka https://play.google.com/store/apps/details?id=com.masangula

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA

For Booking>>> 

EMAIL: yahyamasangula@gmail.com

CALL>>>

Voda: +255742532203
 

JIUNGE NAMI KUPITIA

Download app ya masangulatz hapahttps://play.google.com/store/apps/details?id=com.masangula

No comments